SHEMEJI SIO HUKO EP-5

SEHEMU YA TANO NAYE Aisha hakuwa mbumbumbu, akaupenyeza mkono wake hadi sehemu fulani mwilini mwa Abdul na kushika kile alichotaka kukishika. Akamtomasa kwa mapozi, kiganja chake laini kikizidi kumchanganya Abdul na kumwongezea mhemuko. Hakika Bw. Abdul alipagawa sana hadi kufikia hatua ya kutaka kuvunja amri ya sita ndani ya gari. “Aisha uvumilivu umenishinda mpenzi, tufanye…

SEHEMU YA TANO

NAYE Aisha hakuwa mbumbumbu, akaupenyeza mkono wake hadi sehemu fulani mwilini mwa Abdul na kushika kile alichotaka kukishika. Akamtomasa kwa mapozi, kiganja chake laini kikizidi kumchanganya Abdul na kumwongezea mhemuko. Hakika Bw. Abdul alipagawa sana hadi kufikia hatua ya kutaka kuvunja amri ya sita ndani ya gari.

“Aisha uvumilivu umenishinda mpenzi, tufanye basi hata kidogo,” Abdul alisema kwa tabu, akizidi kumvuta Aisha na kumkumbatia.

Aisha hakuona kuwa ni ustaarabu kufanya mapenzi ndani ya gari hivyo alimshauri shemejiye kuwa wapange siku nyingine ya kufanya maangamizi kunako sita kwa sita.

Kwa kuwa muda ulikuwa umeenda sana hivyo wote walikubaliana kupanga siku nyingine ya kutimiza azma yao.

Huku nyumbani Nasra akiwa juu ya sofa pembeni kuna meza ambayo juu yake kuna glasina chupa iliyojaa juisi ya parachichi. Nasra alimaliza glasi za juisi huku akibadilisha CD za aina mbalimbali kataka runinga.

Muda mrefu ulipita hatimaye Nasra alichoka kukaa kwenye sofa, taratibu alielekea chumbani kujipumzisha huku njaa ikimtafuna. Baada ya saa moja kupita Nasra alishtuka toka usingizini,aliitupia jicho saa iliyokuwa ukutani ambayo iliomwonyesha kuwa ni saa kumi jioni.

“Hee!Sokoni huko sokoni ganijamani tangu asubuhi hadi saa hizi.Mmmm! Haya.Aisha alitamka kwa uchungu.”

Taratibu alivuta mtandio wake na kuupachika begani, kisha akafunga mlango na kuelekea katika baa iliyokuwa karibu na nyumba yaokwa ajili ya kujipatia chochote kitu.

Dakika chache baada ya kurejea nyumbani alisikia sauti ya honi ya

gari iliyoashiria kuwa mumewe alikuwa amerudi.

Nasra alinyanyuka taratibu na kuelekea wanapoegesha gari.

“Vipi jamani wazima?” Nasra aliuliza kwa tabasamu ili kuficha hasira zilizomjaa.

“Sisi wazima dada sijui wewe? Pole sana kwa kukuacha mpweke kwa muda mrefu.” Aisha alitamka kwa furaha ili kuficha upuuzi wake na shamejiye usije ukagundulika.

Usiku ulipowadia walikutana mezani kupata chakula. Nasra kama kawaida yake baada ya dakika chache taratibu alinyanyuka kuelekea chumbani huku akimtakia mdogo wake usiku mwema.

“Na wewe ule haraka tuje kulala.Acheni stori zenu za uongo.” Nasra aliongea kwa utani.

“Sawa bwana.”

Baada ya kimya cha muda mrefu Bw Abduli alianza stori zake za kuwinda ndege.

“Kesho itabidi umuage dada yako kuwa unakwenda kwa rafiki yako Anita ili tuweze kukamilisha mipango yetu,au vipi dear.”

“Sawa usijali.”

Asubuhi ilipofika Aisha hakuona sababu ya kupoteza muda kwani baada ya kumtakia hali dada yake alimweleza juu ya safari yake.

“Dada mimi nataka kwenda kumtembelea rafiki yangu Anita MoorjaniAna nini?Anaumwa?”

“Hapana ninaenda kumtembelea tu”

“Sawa ila jitahidi kumaliza kazi za asubuhi kabla ya kwenda huko”

“Sawa dada.”

Dada’ake hakuwa na kipingamizi kwani hakuelewa kilichokuwa nyuma ya pazia. Hata hivyo alimshauri kuwa asikawie kurudi.Kwani nyakati za usiku huwa kuna uhalifu mwingi.

Bw. Abdul hakuamini macho yake kama siku ile adhimu waliyokuwa wakiisubiri kwa hamu tele hatimaye imewadia.

“Aisha mpenzi unajisikiaje?”Bw. Abdul aliuliza huku akisitasita. Aisha hakujibu lolote zaidi ya kung’ata kucha za vidole na kuangalia dirishani akiashiria kuwa na aibu.

“Nitazame basi mpenzi acha aibu zako wewe! “Ungependa kula nini leo?”

Baada ya kimya cha dakika kadhaa Bw. Abdul aliisogelea simu ilyokuwa mezani na kubofya namba tofautitofauti kisha kuiweka sikioni mwake.

Previous Post

Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Latest News

View All

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

You May Have Missed