SHEMEJI SIO HUKO EP-1

AISHA alijiona kama mtu mwenye bahati kwa kutongozwa na shemejiye. Aliwaza endapo akimkubalia au asimkubalie kwa kuona kuwa ni shemeji yake. Alifikiria sana juu ya utajiri wa shemeji yake na hali aliyonayo yeye . “Endapo nikikubali dada akigundua itakuwaje?” aah!! Lakini si amenitongoza mwenyewe,siwezi kupiga teke fuko la pesa… Potelea mbali.” Siku iliyofuata Aisha alikutana…

AISHA alijiona kama mtu mwenye bahati kwa kutongozwa na shemejiye. Aliwaza endapo akimkubalia au asimkubalie kwa kuona kuwa ni shemeji yake. Alifikiria sana juu ya utajiri wa shemeji yake na hali aliyonayo yeye .

“Endapo nikikubali dada akigundua itakuwaje?” aah!! Lakini si amenitongoza mwenyewe,siwezi kupiga teke fuko la pesa… Potelea mbali.”

Siku iliyofuata Aisha alikutana na rafiki yake aliyeitwa Anita. Aisha alimsimulia Anita kuhusu shemejiye.

“Shoga basi ngoja nikupe mkanda”.

“Hapo ndipo ninapokupendea tukikutana baraza huchangamka kwa stori, haya shoga hebu nipe huo mkanda”.

“Jana usiku wakati tunakula,dada aliwahi kushiba akaenda zake kulala, sebuleni tukabaki mimi na shemeji tukipata dinna. Basi shoga’angu shemeji si nd’o akaanza… Ooh Aisha unajua wewe mzuri sana kuliko hata dada’ko mi nikabaki kucheka tu. Dakika chache zikapita mara akaanza tena… Aisha najua wewe ni mtu mzima unayeweza kutunza siri,mi nataka we uwe mpenzi wangu lakini dada’ko asijue. Shoga nlishtuka kwani sikutegemea hata sikumoja kama shemeji atakuja kunitamkia maneno kama yale, ukizingatia jinsi ninavyomheshimu.” “Heehee shuntu babuu ….. Aaa babu wee heshima hiyo kwani baba’ko mzazi yule.” Anita alidakia, wote kwa pamoja waliangua vicheko vya umbea.

“Sasa sikiliza shoga yangu nikwambie maisha ndo hayo yanaanza kukunyookea ukizingatia shemejiyo alivyo na utajiri,kuuacha ni sawa na kukataa kuolewa na mfalme ili uje kuwa malkia”.

“Kwa hiyo ndo unaniambiaje?”

“ Hee bibi ee tulia mbona una haraka kama mkojo wa asubuhi,utakukurupua kitandani utake usitake,usiombe ukakuta chooni kuna mtu utaisoma, utarukaruka kama umepewa adhabu na mwalimu. Kama kakuanza mwenyewe basi kamaindi figa huyo.

Vibaya kama umemuanza wewe au umemtega? Maana na sisi wanawake hatujambo.Ukimpenda mwanamume utamfanyia kila visa hadi ataingia laini mara urembue macho,mara umvalie khanga moja na hiyo mikalio yako shoga kama umemfanya hivyo mwanamume wa watu utamuua.”

“ Acha utani Anita”

“Basi ndo hivyo shoga’angu.”

“Mimi jana nilimwambia angoje nifikirie maana niliishiwa pozi, nkashindwa hata kuongea. Taratibu nlielekea chumbani kwangu na kuanza kufikiria. Mpaka leo asubuhi sikupata jibu, nlijumlisha na kutoa lakini jibu halikupatikana. Lakini sasa nimepata jibu zuri nd’o ma’na nakupenda hapo hapakosi jibu la uhakika,ama kweli we ndo jembe langu”.

“Aisha”

“Abee” Aisha aliitika na mazungumzo yao yalikatishwa na wito ule, hivyo kila mmoja alielekea kwao.

”Kachukue pesa juu ya meza wende sokoni.Unataka kumpikia nini leo shemejio?”

“Mi si ninajua shemeji yangu anapenda wali na samaki, basi nami ntapika hivyo.”

“Haya nenda basi.”Nasra alimsihi Aisha ambaye alikuwa akitoka kuelekea sokoni.

Akiwa njiani Aisha alijawa na mawazo juu ya shemeji yake, alifikiri kama shemeji yake alimpenda kweli au alimtega tuu ili

kupima imani yake.“Atajijua mwenyewe, mimi leo akiniuliza nitamwambia nimekubali. Kama lengo lake ni kunipima imani yangu basi atapata robo kilo.”

Aliwaza Aisha ambaye tayari alikuwa ameshafika sokoni na kuchukua mahitaji aliyoagizwa.

Kama kawaida yao usiku ulipowadia chakula cha usiku kilikuwa tayari mezani na wote watatu walikutana mezani kwa ajili ya kupata msosi.

“Mume wangu, leo Aisha amesema shemejiye wapenda sana wali kwa samaki ndiyo maana ameamua kukupikia.” Nasra alisema kwa utani bila ya kujua kinachoendelea. Wote walicheka.

“Kumbe ndiyo maana chakula cha leo kitamu. Kumbe hii ni spesho dinna for me?” Bwana Abduli alitabasamu huku akimwangalia

Previous Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Latest News

View All

About the Author

Easy WordPress Websites Builder: Versatile Demos for Blogs, News, eCommerce and More – One-Click Import, No Coding! 1000+ Ready-made Templates for Stunning Newspaper, Magazine, Blog, and Publishing Websites.

BlockSpare — News, Magazine and Blog Addons for (Gutenberg) Block Editor

You May Have Missed